Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu: Niliwahi kuwa dancer

Skudo Mweh Skudo: Niliwahi kuwa dancer

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela Manoka 'Skudu' raia wa Afrika Kusini kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa alishawahi kuwa dancer wa muziki nchini kwao ndiyo maana ana uwezo mkubwa wa kucheza.

Skudo aliyekuwa akikipiga Marumo Gallants amesema kuwa ameheshimishwa kupewa jezi hiyo na ni deni kwake kuitendea haki ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga kwa kusaidiana na wachezaji wenzake kuiletea mafanikio zaidi klabu hiyo.

"Nilishawahi kuwa dancer, na soka lina vitu vingi, mchezaji unahitaji kutengeneza muunganiko na mashabiki zako. Tumepewa vipaji tofauti, kwa hiyo kama unaweza kufanya jambo flani kwenye mpira tunasema umepewa kipaji hicho na Mungu, ni kipaji.

"Kwa hiyo ninachokifanya ni kutumia kipaji change nilichopewa na Mungu ili kukirudisha kwa mashabiki wanaokubali kile ninachokifanya ili wafurahie. Soka ni mabao na kushinda, kwa hiyo ukitumia kipaji chako kuipa ushindi timu yako linakuwa ni jambo jema.

"Baada ya kucheza hapa niliona video yangu ikitrend hapa Tanzania, sikujua ni kwa nini lakini baaadaye mashabiki wa Tanzania wakaanza kunifuata mtandaoni na kuniambia wanatamani nije kucheza hapa, mipango ya Mungu ndiyo imetimia.

"Ninawaomba mashabiki tuungane, tupambane tena msimu huu ili kubakisha mataji yetu ya ndani tuliyoshinda msimu uliopita na kufanya vizuri zaidi kimataifa. Siwezi kusubiri kuingia uwanjani na kuwapa furaha mnayoitarajia kutoka kwangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu, asanteni wananchi," amesema Skudo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: