Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu Makudubela aingia kwenye rada za APR

Skudu Makudubella Winga wa Yanga, Skudu Makudubela

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya APR ya Rwanda imevutiwa na huduma ya nyota wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na tayari imefanya mazungumzo naye ili aweze kwenda kuiongezea nguvu timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano nchini humo na anga la kimataifa.

Skudu aliyejiunga na Yanga mwaka jana akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini baada ya kuvutiwa naye zilipokutana katika mechi za nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, japo amekuwa hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Miguel Gamondi jambo linalowavutia mabosi wa APR kuihitaji saini yake ili atue kikosini.

Mabingwa hao wa Rwanda, wanaamini mchezaji huyo atakuwa msaada kwa kikosi hicho hasa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ila itakumbana na upinzani mkali kwani timu mbalimbali pia zinamtaka ikiwemo Magesi FC iliyopanda daraja Afrika Kusini.

Skudu ni mmoja ya wachezaji wanaotajwa kuondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba, akiwa ameifungia mabao mawili, likiwamo moja ya Ligi Kuu Bata na jingine la Kombe la Shirikisho, huku akiwa ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kutokana na kupita klabu kadhaa zikiwamo za kwao Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: