Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu: Hizi ni mechi tano za kufia uwanjani

Skudu Makudubella Skudu Makudubela.

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mechi tano zilizobaki za Ligi Kuu ya NBC, nyota wa kikosi cha Yanga, Skudu Makudubela amesema wao kama wachezaji watazicheza mechi hizo kama fainali kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri.

Skudu ameyasema hayo wakati huu ambao Yanga wamebakiwa na mechi tano za kumaliza msimu huku tukiwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa.

“Kila mechi inayokuja kwetu ni kama fainali, tunafahamu mashabiki wanachokitarajia kutoka kwetu, tuna mtihani uliopo mbele na tunajitoa kwa asilimia mia kila mchezo kwa sababu yote ni muhimu.

“Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kutusapoti na waendelee kufanya hivyo mpaka mwisho, tunawaahidi tutapambana kuwapa furaha,” alisema Skudu.

Katika mechi tano zilizosalia, Yanga wanaanza leo Jumatano kucheza Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Kagera Sugar, saa 1:00 usiku. Baada ya hapo, watakwenda ugenini mkoani Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar, kisha Dodoma kupambana na Dodoma.

baadaye watarejea nyumbani kukabiliana na Tabora United halafu watamaliza dhidi ya Tanzania Prisons ambapo katika mechi hizo tano zenye pointi 15, wanahitaji 8 pekee kuwa mabingwa mara 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live