Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudo ataweza kuvaa viatu vya Fei Toto Yanga?

Fei Toto Skudo Skudo ataweza kuvaa viatu vya Fei Toto Yanga?

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye uongozi wa Young Africans Sports Club umekata kiu ya mashabiki wake kwa kumtambulisha nyota mpya atakayevaa jezi namba 6 msimu ujao.

Ikumbukwe kwamba jezi hiyo ilikuwa mikononi mwa Feisal Salum ambaye yeye msimu ujao hatakuwa ndani ya Yanga bali Azam FC.

Ni nani huyu? Ni winga mwenye kipaji kikubwa cha mpira kutoka Ardhi ya hayati Nelson Mandela, Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela, maarufu kama Skudu.

Nyota huyu mwenye uwezo mkubwa wa kucheza na mpira akiwa na ufanisi wa kutumia miguu yake miwili, amejiunga na Yanga kama mchezaji huru baada ya kuachana na timu yake ya Marumo Gallants.

Skudu alianza soka lake kwenye mitaa ya Soweto, kabla ya baadae kuchukuliwa kwenye kituo cha soka cha Mamelodi Sundowns kabla ya baadae kujiunga na Orlando Pirates.

Timu nyingine ambazo amewahi kupita Skudu ni Highlands Park, Chippa United, Golden Arrows, Platinums Stars na Marumo Gallants.

Msimu uliopita Skudu alikuwa sehemu ya kikosi cha Marumo kilichofanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, kwa kufika hatua ya Nusu Fainali na kuondolewa na Yanga kwa jumla ya mabao 4-0.

Skudu amekuwa mchezaji wa sita kutambulishwa Yanga, baada ya Nickson Kibabage, Jonas Mkude, Gift Fred, Maxi Nzegeli na beki Yao Koaussi kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Julai 22 Yanga ina mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Wiki ya Mwananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: