Shirikisho la soka Uhispania (RFEF) limetangaza kumfuta kazi meneja wa timu ya Taifa ya Wanawake, Jorge Vilda ambaye aliiongoza Timu ya Wanawake ya Uhispania kutwaa kombe la Dunia la Wanawake 2023.
Hatua hiyo imefanywa na bodi mpya ya RFEF iliyoundwa baada ya FIFA kumsimamisha Rais Luis Rubiales kufuatia kitendo chake cha kumbusu mchezaji Jennifer Hermoso.
Vilda ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Rubiales, amekuwa akikabiliwa na mzozo tangu mwaka jana baada ya wachezaji 15 kumtaka ajiuzulu kwa sababu ya mbinu zake duni za kufundisha.
Mbinu za kocha huyo zimedaiwa kutaka masharti ya kikosi cha Wanawake yalingane na yale ya kikosi cha wanaume.