Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siwa ataja pakuanzia kwa makipa Yanga

Reorganize Ed 0 Siwa ataja pakuanzia kwa makipa Yanga

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Siwa alisema hana shida na uwezo wa makipa hao kwa sababu amekuwa akiifuatilia Yanga ilipocheza michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na Ligi Kuu na kubaini pa kuanza kufanyia kazi.

“Sina shida kabisa na makipa waliokuwapo sasa Yanga, wana uwezo mkubwa, kuna vitu ambavyo wanavikosa na mara nyingi nimepata kushuhudia mechi walizocheza na kuona makosa wanayoyafanya, nina imani nitawasaidia na kufikia malengo yetu,” alisema Siwa.

Alisema ameona mazingira ya kambi ya timu hiyo, kwa kushirikiana na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi, watafanya vizuri, hivyo kikubwa ni kuhakikisha wanashinda mechi zao bila kuangalia nyuma, mwenzao anafanya kitu gani.

“Nina imani kubwa Yanga ina nafasi ya kuchukuwa ubingwa endapo tutaungana kwa pamoja na kuhakikisha kila mechi iliyopo mbele yetu tunahitaji kupata ushindi bila kumfikiria anayetukimbiza ameshinda bao ngapi au amepoteza michezo yake,” alisema Siwa.

Chanzo: ippmedia.com