Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sitarajii kuona usajili wa kushtua - Kiemba

Sitarajii Kuona Usajili Wa Kushtua   Kiemba Sitarajii kuona usajili wa kushtua - Kiemba

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Amri Kiemba, amesema kuelekea kwenye usajili wa dirisha dogo, hatarajii kuona usajili wa kushtua.

Aamesema wengi wanaosajiliwa kipindi hiki ni wale ambao wanahitaji tu kubaki kwenye ligi kuu na sio vinginevyo.

“Mimi sitarajii kuona usajili wa kushtua lakini kuna usajili unaweza kufanyika ukawa na tija kwenye klabu, mfano sio lazima yajae majina makubwa kwenye klabu.

“Usajili wa dirisha kubwa ndio wakati ambao wachezaji wengi wanapatikana, dirisha hili unaweza kuchukua mchezaji ambaye malengo yake ni kubaki kwenye ligi tu au kwenye klabu yake hawamuhitaji na pengine klabu ione huu ndio wakati wa kumuuza ili mwisho wa msimu asije kushuka,” alisema Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live