Wakati usajili wa Dirisha Dogo ukiwa umefunguliwa Barani Ulaya, wachezaji wengi wanakwenda kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, hivyo hivi sasa wamebakiwa na miezi sita pekee.
Klabu ya Real Madrid, ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wanakwenda kumaliza mikataba yao, tena ni wale wanaounda kikosi cha kwanza.
Wachezaji wanne ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu ni Toni Kroos, Luka Modric, Nacho Fernandez na Lucas Vazquez, huku majadiliano kuhusu mikataba mipya yakiripotiwa kuanza kufanyika.
Wakati nyota hao wanne mikataba yao ikienda ukingoni, Kepa Arrizabalaga na Joselu Mato wanacheza hapo kwa mkopo, nao msimu ukimalizika wanarudi kwenye klabu zao, hivyo kufanya idadi ya wachezaji sita wa kikosi cha kwanza ndani ya Madrid wanaweza wasiwepo msimu ujao.