Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita kutemwa Madrid

Hazard And Asensio Marco Asensio na Eden Hazard ni miongoni mwa Wachezaji wanaotazamiwa kutemwa Madrid

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid imepanga kupunguza mzigo wa wachezaji ili kupisha nafasi ya wachezaji wapya ambao klabu inapanga kuwasijili kwenye majira ya kiangazi huku Eden Hazard na Marco Asensio yakiwa majina makubwa ambayo yanatarajia kuonyeshwa njia.

Real Madrid wamepanga kufanya matumizi makubwa kwenye dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, baada ya Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kutaka kufanya usajili wa majina makubwa wakiwemo Mbappe na Haaland kama usajili wao wa kwanza muhimu.

Wachezaji ambao siku zao za kubakia kwenye kikosi cha Los Blancos zinahesabika, ni Eden Hazard ambaye amekuwa akisumbuliwa na mejeruhi ya mara kwa mara tokea asajiriwe na klabu hiyo, Marco Asensio nae ataonyeshewa mlango wa kutokea.

Ukiachana na majina hayo makubwa kwenye kikosi cha Real Madrid, wengine ni washambuliaji wa kati Luka Jovic na Mariano Diaz nao wapo kwenye list ya kuondolewa, pia kiungo Dani Ceballos, ambaye anahitajika na klabu yake ya zamani ya Real Betis na mlinzi Jesus Vallejo nae ataoneshewa njia ya kutokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live