Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita Man United kuwakosa Chelsea

Sic Players Meneja wa United akiwa Uwanja wa Mazoezi

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick amethibitisha wachezaji 6 watakosekana katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo utakaopigwa Old Trafford hapo kesho.

Manchester United wanaingia katika mchezo huo wakiwa wametoka kupoteza mbele ya Arsenal kwa magoli 3-1 wikiendi iliyopita walipoenda kuwatembelea Gunners kule Emirates.

Rangnick amesema wachezaji watakaokosekana ni pamoja na kapteni, Harry Maguire, Paul Pogba (aliyeumia katika mchezo uliopita), Fred, Edinson Cavani, Luke Shaw na Jadon Sancho.

United bado wanatetea ndoto za kumaliza katika nafasi nne za juu ili kuweza kucheza michuano ya ulaya msimu ujao lakini wanakabiliwa na kibarua kizito kutokana na majeruhi na ubora wa wapinzani wao.

Katika mchezo wa kwanza waliokutana msimu huu, United walifanikiwa kuondoka na alama moja katika dimba la Stamford Bridge baada ya kupata sare ya 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live