Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita Championship zapenya 32 Bora ASFC

Hampionship Pic Sita Championship zapenya 32 Bora ASFC

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Achana na matokeo ya mechi za juzi za raundi ya pili ya michuano ya ASFC, hadi juzi ni timu sita tu kati ya 12 zilizofuzu kwenye raundi ya tatu ya michuano hiyo ambayo bingwa wake uiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Raundi hiyo ya pili ilishirikisha timu 64 zinatakazochujana na kubakisha 32 na utepe ulianzwa kwa Silent Ocean iliyoialika Copco ya Championship iliyotakata kwa ushindi ugenini wa 3-2 na kuwa timu ya kwanza kufuzu raundi ya tatu.

Timu nyingine iliyofuzu hatua hiyo, ni Gwambina iliyoitandika Nduguti Stars kwa 3-1 kwenye uwanja wake wa Liti Singida, huku Mbuni iliyocheza michezo mitano mfululizo ya Championship bila ya ushindi ilifanya kweli kwa kuinyoa African Lyon kwa penalti 3-1 baada ya dakika 90 kufungana 2-2.

Maafande wa Green Warriors wakiwa kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, jijini Dar es Salaam ilifuzu raundi ya tatu kwa kuitungua Stand United kwa penalti 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Vinara wa Ligi ya Championship, JKT Tanzania ilipindua meza baada ya kutanguliwa bao 1-0 hadi dakika ya 88 ya mchezo na kufanya ‘comeback’ ya kibabe na kupindua matokeo mwishoni baada ya kuifunga Biashara United mabao 2-1.

Mashujaa ikiwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ilipa kisasi cha kufungwa 2-0 na Pamba Novemba 26 katika Championship baada ya kuifunga 3-1 na kuitoa mashindanoni.

Akizungumza Kocha Mkuu wa Gwambina, Khassain Salum alisema michezo hii huwa ni migumu kwa sababu ni ya mtoano na unacheza na timu ambazo haujia aina ya uchezaji wao, huku Kocha Mkuu wa Mbuni, Leonard Budeba alisema ushindi walioupata ni wa fahari kutokana na kucheza vizuri na kwa nidhamu kwani anaamini ni njia ya kurejesha ari ya timu yake.

Chanzo: Mwanaspoti