Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sisi ndio wawakilishi pekee wenye uhakika wa kufanya vizuri Kimataifa – Kamwe

Ally Kamwe 10 K Ticket Sisi ndio wawakilishi pekee wenye uhakika wa kufanya vizuri Kimataifa – Kamwe

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ally Shaban Kamwe ambaye ni Afisa Habari wa Yanga Africans, ametamba kuwa, wao ndio wawakilishi pekee wa Kimataifa wenye uhakika wa kufanya vizuri kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kamwe ameyasema hayo leo Septemba 12, 2023 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi Media kuhusu mipango yao kuelekea mchezo wao wa hatua ya kwanza dhidi ya Al Merrikh.

“Tunaweza kuwa tupo wengi darasani lakini sisi pekee ndio tuna uhakika wa kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika,” alisema Ally.

Msemaji huyo alisema anatamka hivyo mapema kwani kila kitu kimejidhihirisha mapema kabisa, Yanga wameanza kutwaa tuzo za mwezi Agosti ambapo kocha bora na mchezaji bora ametokea kwenye kikosi chao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live