Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri ya straika wa Maurtania kuitwa jina bunduki

Ak 47 Pic Siri ya straika wa Maurtania kuitwa jina bunduki

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Maurtania, Aboubakar Kamara amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kwa siku ya jana baada ya jina lake kwenye orodha ya kikosi ambacho kimeanza kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso, kusomeka AK-47.

Katika taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Maurtania kupitia mitandao yao ya kijamii ilionyesha staa huyu anasomeka AK-47 ambayo ni aina ya bunduki kutoka nchini Urusi.

Wengi walishangazwa na hili lakini ukweli ni kwamba AK ni kifupisho cha jina lake la Aboubakar Kamara kisha 47 ni namba ya jezi ambayo huwa anavaa kwenye klabu anazochezea.

Kwa upande wa timu ya taifa staa huyu ambaye aliwahi kucheza Fulham kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 anavaa namba 27.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live