Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri ya FA kusubiri mwaka mzima kuajiri kocha mpya ni hii

Carsey Siri ya FA kusubiri mwaka mzima kuajiri kocha mpya ni hii

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

CHAMA cha soka cha England kimepanga kusubiri kwa mwaka mzima kabla ya kuajiri kocha mpya atakayechukua mikoba ya Gareth Southgate aliyejiuzulu hivi karibuni na nafasi yake kuchukuliwa na Lee Carsley ambaye alikuwa ni kocha wa timu za vijana.

Inelezwa moja kati ya mambo yaliyofanya FA iamue kusubiri kwa karibu mwaka mzima ni kutaka kujipa muda kumtazama kocha wa mpito Carsley mwenendo wake na kama itaridhishwa naye basi itampa mkataba wa moja kwa moja kuifundisha timu hiyo.

Vilevile, FA inafanya hivyo ikiamini mwisho wa msimu ujao itakuwa rahisi kupata makocha inaowahitaji kama Eddie Howe na Pep Guardiola atakayekuwa anamaliza mkataba wake na Manchester City.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Sun ni kwamba baadhi ya viongozi wa juu wa FA wanaamini kocha wa timu ya vijana ambaye ndiye kocha wao wa mpito kwa sasa anaweza akamudu vyema jukumu hilo, hivyo watampa muda wa kumtazama kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Utaratibu huu unaotaka kutumika sasa ndio uliotumika kwa Southgate ambaye alipewa nafasi ya kuwa kocha wa mpito mwaka 2018 na baada ya kufanya vizuri kwa miaka kadhaa, akapewa mkataba wa kudumu wa kuitumikia timu hiyo.

Baadhi ya viongozi wengine wanaamini mbadala wa Southgate ambaye ameondoka siku kadhaa baada ya kupoteza ubingwa wa Euro mbele ya Hispania ni Guardiola. Hadi sasa hakuna uhakika ikiwa Pep ataendelea kuifundisha Man City baada ya msimu ujao ama ataondoka kwa sababu licha ya kufanya mazungumzo na mabosi wa timu hiyo hawakufikia muafaka wa kusaini mkataba mpya.

Carsley amefanya vizuri akiwa na timu ya England ya vijana wenye umri chini ya miaka 21, na mwaka jana aliisaidia kushinda Kombe la Euro mbele ya Hispania kwa bao 1-0.

Chanzo: Mwanaspoti