Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri nyimbo za Taifa kufanana

Taifa Stars Link Siri nyimbo za Taifa kufanana

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fainali za Afcon 2023, zinaendelea Ivory Coast katika miji mitano na wengi wanafuatilia zikiwa zinakaribia kumaliza hatua ya makundi kuanzia mechi za leo.

Jana katika mchezo wa kundi F, Zambia dhidi ya Tanzania kwenye Uwanja wa Laurent Pokou San Pedro, zilipigwa nyimbo za taifa za nchi hizo na huenda wengi walijiuliza mengi baada ya kuzisikiliza kutokana na kufanana kwao.

Je mtunzi wa nyimbo ni mmoja?

Ndio mtunzi wa nyimbo ni mmoja, raia wa Afrika Kusini, Enoch Sontonga, aliyekuwa kasisi wa Xhosa kutoka shule ya wamishonari ya Methodist, Johannesburg.

Enoch alitunga wimbo wa “Nkosi Sikelel’ iAfrika” wenye maana ya 'Mungu Ibariki Afrika' mwaka 1897 na ulitungwa kwa lugha ya kixhosa na mwaka 1927 uliongezewa mistari saba na mshairi Samuel Mqhayi.

Ulitumiwa kama wimbo wa chama cha African National Congress (ANC), kipindi cha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na ulikuwa kama alama ya harakati za upingaji wa ubaguzi wa rangi.

Hata hivyo, ulitumika ingawa sio rasmi kama wimbo wa taifa wa nchi hiyo kabla ya makaburu waliokuwa wakiitawala nchi hiyo kuupiga marufuku kutokana na kuhusishwa na chama cha ANC.

Wimbo huu unaotumiwa na mataifa matano, unafanana kibwagizo cha 'Nkosi Sikelel iAfika' huku mashairi yakitofautiana ingawa maudhui ni yale yale na hata staili unavyouimbwa na melodi zinafanana kwa kiasi kikubwa.

Ulitumika kama wimbo wa ukombozi wa Afrika, kabla baadaye nchi kadhaa kukubaliwa kutumia kama wimbo wa taifa na nchi tano ziliutumia zikiwamo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baadaye Afrika Kusini baada ya kupata uhuru ulipomalizika ubaguzi wa rangi.

Melodi ya wimbo huo bado unatumikwa kwenye nyimbo za taifa za Tanzania na Zambia huku Zimbabwe, Namibia zenyewe baadaye zilibadilisha melodi na mashairi ya nyimbo zao.

Unavyoitwa na nchi hizo

Tanzania - "Mungu Ibariki Afrika" tangu mwaka 1961.

Zambia - "Nkosi Sikelel' iAfrika" tangu mwaka 1964 hadi 1973 baada ya kubadilishwa melodi na kupewa jina lingine la "Stand and Sing of Zambia, Proud and Free".

Namibia - "Nkosi Sikelel' iAfrika" ulitumika kama wimbo wa taifa wa nchi hiyo kipindi cha kupata uhuru, Machi, 1990, lakini baadaye ulibadilishwa na kuitwa "Namibia, Land of the Brave" na uliimbwa kwa mara ya kwanza kwenye maadhimisho ya kwanza ya siku ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1991.

Zimbabwe - "Ishe Komborera Africa" ndio ulivyoitwa nchini huko na ikiwa na maana 'Mungu Ibariki Afrika' na uliimbwa kwa lugha ya Shong na Ndebele na ndio ulikuwa wimbo wa kwanza wa taifa hilo tangu uhuru mwaka 1980.

Ulibadilishwa mwaka 1994 na kuwa "Ngaikomborerwe Nyika yeZimbabwe/Kalibusiswe Ilizwe LeZimbabwe" kwa lugha ya Kiingereza ukimaanisha "Blessed be the land of Zimbabwe", hata hivyo wimbo huo wa kwanza "Ishe Komborera Africa" bado ndio maarufu nchini humo.

Chanzo: Mwanaspoti