Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sioni kosa la Fei kuwanyamazisha mashabiki wala mashabiki kumzomea

Fei Toto 0001 Sioni kosa la Fei kuwanyamazisha mashabiki wala mashabiki kumzomea

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binafsi sioni kosa la Mashabiki wa Yanga kumzomea Maestro Feisal Salum jana na bado sioni kosa kwa Feisal kuweka penati kambani na kuwanyamazisha Mashabiki jana, huo ndio mpira wa miguu tangu zama hizo yani una raha na karaha, jeuri na ubabe wake.

Kinachoendelea naona kuna chuki ya KULAZIMISHWA kutoka nje ya Feisal na Yanga inajaribu kujengwa kati ya FEISAL na YANGA, sioni kama kiuhalisia Yanga wana chuki yoyote na Maestro! Umewahi kusikia sehemu wamempiga huko mtaani? Umewahi kusikia wamemfanya kitu kibaya huko mtaani? Jibu ni HAPANA.

Brothers and Sisters mpira wa miguu huu ndio utamu wake, watu ni vichaa haswa! Nadhani tulipaswa kuwapongeza sana Mashabiki wa Yanga na Yanga kiujumla kama taasisi lakini pia Maestro Feisal, wote wawili wamekubali yameisha kati yao na kila mmoja anaendelea na maisha yake, ulisikia katupiwa kopo la maji ama kupigwa jana? Jibu ni HAPANA.

Mwisho wa siku hakuna aliyepoteza kati yao! Yanga ameendelea kuzoa medali kama kawaida yake na Feisal ameendelea kuwa kwenye ubora wa juu kama kawaida yake, mwisho wa siku ni vita ya kimalengo na kila mmoja anashinda mechi zake tena vizuri sana, nani kapoteza kati ya Feisal na Yanga? Hilo majibu mimi sina na yako baki nayo.

Karejeeni vyema kwenye mkasa wa Luis Figo pale Netflix inaitwa Casa del Figo, ndipo utaelewa ukatili na uadui kwenye mpira baada ya yeye kuondoka Barcelona na kujiunga na Madrid, ila Feisal na Yanga ni upendo kati yao uliojificha katika chuki wala hawana tatizo hawa ila kuna namna watu wanalazimisha.

For the good of the game! Mwisho wa siku career ya Maestro Feisal itahukumiwa kwa makombe na tuzo binafsi, hivyo ndivyo Wachezaji wakubwa hupimwa! Kila la heri kwa Yanga na kwa Maestro Feisal Salum, a match made in heaven, mnapendana sana, si ajabu siku Feisal akarudi Jangwani na watamshangilia ndio Football.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live