Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio wazawa tu, hata wageni wamefeli!

Okrah Ndani Sio wazawa tu, hata wageni wamefeli!

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado kuna changamoto ya mazoea kuwa timu zetu LAZIMA zisajili Wachezaji wa kimataifa tu na sio Locals (Wazawa) ni mara ngapi Wageni wakaja na wakafeli? Je hakuna Wazawa waliofaulu?

Simba aliwahi kuchukuwa Wazawa wanne Azam na akafaulu nao sana, Azam alibeba ubingwa akiwa na wazawa wengi tu, Yanga ana Wazawa ambao ni top talents pia.

Kwanini tukariri kuwa timu zetu ili zifanye vyema lazima zisajili nje tu? Wakina Shomari, Zimbwe, Job, Mwamnyeto, Aishi, Mzamiru walipatakanaje? I believe wapo Wachezaji wana uwezo wa kuperform hizi timu kubwa na tusiwaze waliofeli tu.

Wapo wachezaji wa Kimataifa walianza kwa kufeli ila wakapewa muda wakaonesha uwezo mkubwa sana, hizi timu zetu Viongozi wasipewe presha kubwa na wao wasiishi kwa presha waende sokoni kutazama wabora kwenye kila eneo kama ni Mtanzania basi apewe nafasi bila kuogopa.

Yupo wapi aliyewaza kuhusu saini ya Hassan Dilunga HD? Ikalipa ni Mzawa! Yupo wapi aliyewaza saini ya Dickson Job? Ikalipa ni Mzawa, kama ilivyo kwa Kichuya Shiza na Zawadi Mauya! Suala ni technical report inataka nini.

Haipaswi kuwa vita timu ikitaka Mchezaji wa ndani, mara ngapi kimataifa wamekuja vituko hapa? Tuwaamini na Vijana wetu pia, under proper coaching wanashine sana! Feisal Salum wa JKU sio wa Yanga, Zimbwe wa Kagera sio wa Simba its all about Coaching na unacheza na nani.

Wageni baadhi wana viwango bora sana na wamesaidia sana kuongeza ushindani kwenye mpira wetu kuanzia uwanjani mpaka kwenye maslahi, ni kitu kizuri nasi tunapenda wakija wawe na viwango kweli sio suala la kupanda tu ndege????

Chanzo: www.tanzaniaweb.live