Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio riziki! Mastaa hawa walifeli usajili kisa vipimo

Fekir Ear Nabil Fekir

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Dirisha la usajili la majira ya baridi mwaka huu lilifungwa juzi ambapo kumekuwa na sajili mbali mbali zilizofanikiwa na zile ambazo hazikufanikiwa.

Mbali ya masuala ya pesa moja kati ya mambo ambayo huwa yanakwamisha sajili mbali mbali mara nyingi huwa ni vipimo vya afya ambapo baadhi ya wachezaji huwa wanafeli.

Ingawa katika dirisha hili suala hilo halijatokea lakini mara kadhaa madili yamekuwa yakikwamishwa na mambo hayo hususani katika siku za mwisho za dirisha. Hawa hapa wachezaji watano waliofeli kujiunga na timu husika baada ya kufeli vipimo katika dakika za mwisho.

Ruud van Nistelrooy

Suala la kufunga kwake lilikuwa kama kula keki tu. Alilifanya goli jinsi alivyotaka wakati huu alikuwa akiichezea PSV, kocha wa Manchester United wa wakati huo Sir Alex Ferguson akavutiwa na kiwango chake na mazungumzo ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2000.

Tayari kila kitu kilikuwa kwenye mstari, dili hilo linadiawa kuwa lingekamilika kwa Man United kutoa Pauni 19 milioni ambayo ingeenda kuvunja rekodi yao ya usajili.

Man United ilishandaa hadi siku ya kumtambulisha fundi huyo lakini mwoshowe dili lilifeli baada ya fundi huyo kufeli vipimo vya afya kwa kugundulika kwamba alikuwa na majeraha ya goti.

Hata hivyo Man United ilikaa tena mezani mwaka mmoja baadaye na kumsajili fundi huyo kwa kiasi hicho cha pesa.

Radamel Falcao

Staa huyo wa kimataifa wa Colombia alisajiliwa na Chelsea baada ya kuwa naa wakati mgumu katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Mambo hayakwenda vizuri pia akiwa na Chelsea ambapo Monaco ikatuma ofa ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya baridi mwaka 2016.

Falcao akatua nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya katika siku ya mwisho ya dirisha lakini mambo yalikuwa magumu baada ya kufeli vipimo na dili hilo likafa.

Makamo mwenyekiti wa Monaco baada ya kufeli kwa dili hilo alisema, Vadim Vasilyev :“mpango wa kwanza ulikuwa ni kumsajili Falcao amalize nusu ya msimu huu akiwa na sisi lakini kwa bahati mbaya alikuwa na majeraha hivyo imeshindikana."Falcao alisalia Chelsea kumalizia msimu na mwisho wa msimu akatua Monaco.

Nabil Fekir

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2018 ,Liverpool ilikuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa staa wa Olympique Lyon Nabil Fekir kwa ada ya uhamisho wa Pauni 53 milioni .

Liverpool ilifanikiwa kufikia makubaliano Baada ya kushinda vita dhidi ya Manchester City na timu nyingine nchini England, jamaa akakamilisha hadi baadhi ya taratibu na alishawasili hadi Jijini Liverpool ambapo alifanyiwa utambulisho kupitia Liverpool TV.

Lakini mambo yalishindikana kwa sababu staa huyo alifeli vipimo baada ya kugundulika kuwa ana majeraha ya goti.

Loic Remy

QPR ilishakubali kushindwa na kuamini kwamba mshambuliaji wao huyu angeenda Liverpool kwani makubaliano yote yalishafikiwa muafaka. Lakini dili hilo likafeli katika dakika za mwisho na Chelsea ikatumia mwanya huo kumsajili Remy ambaye alienda kuwa mmoja kati ya wachezaji wao muhimu.

Remy alishawasili hadi kwenye uwanja wa mazoezi wa Liverpool na akafanya mazoezi na timu hiyo kabla ya dili lake la Pauni 8.5 milioni kukamilika.

Baada ya dili hilo la kwenda Liverpool kufeli Remy mwenyewe alisema:"Waliwasiliana na wataalamu wa masuala ya moyo ambao baada ya kunifanyia vipimo vya afya wakasema kwamba hawana uhakika namimi kwa asilimia mia."

Marko Arnautovic

Chelsea ilikuwa inataka kumsajili katika dirisha la majira ya baridi mwaka 2009 wakati huo akiwa na FC Twente, lakini katika dakika za mwisho dili halikutiki baada ya staa huyo kufeli vipimo vya afya.

Wakala wa staa huyo Robert Groener alisema licha ya dili kufeli Chelsea haikuonyesha kufanya jitihada zozote.

Baada ya kushindwa kutua kwa wababe hao Arnautovic alijiunga na Inter Milan kwa mkopo kwenda Inter Milan kisha akajiunga na Werder Bremen na alitimiza ndoto yake ya kucheza England mwaka 2013 alipotua Stoke City.

Chanzo: Mwanaspoti