Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio alizeti, Singida BS wanavuna mpaka pointi

Bruno Gomes Text Friend Singida BS

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania, hilo lipo wazi kutokana na asilimia kubwa kuwekeza kwenye kilimo.

Wapo wale Singida Big Stars wapo ndani ya ligi ambao wanatokea mkoa ambao unafanya kilimo cha alizeti, lakini wenyewe hawavuni alizeti tu za Singida bali mpaka pointi tatu, na hapa tupo nao kwenye mwendo wa data namna hii;

DAKIKA 2,160 Imecheza jumla ya mechi 24 za ligi ambazo ni dakika 2,160 msimu huu ikiwa imekusanya jumla ya pointi 47 kibindoni.

Ina wastani wa kusepa na pointi tatu kila baada ya dakika 720, kwenye mechi ambazo wanacheza iwe nyumbani ama ugenini.

KICHEKO DAKIKA 1,260 Tabasamu halisi la wachezaji wa timu hiyo la kusepa na pointi tatu limeonekana kwenye mechi 14 ambazo ni dakika 1,260 walipowatungua wapinzani wao.

Miongoni mwa timu ambazo zimeonja joto ya jiwe la Singida BS ni Azam FC ambao walitunguliwa bao moja na Bruno Gomez kwa pigo la faulo ilikuwa Januari 23, 2023.

Kagera Sugar nje ndani, wametunguliwa na Singida ndani ya dakika 180 na kuwapatia zawadi ya pointi sita wakulima hao wa alizeti.

NGOMA NZITO DAKIKA 450 Wagumu pia kutunguliwa kutokana na ukuta kuongozwa na wachezaji wenye uzoefu ikiwa ni Pascal Wawa ambaye aliwahi kucheza ndani ya Simba.

Ni mechi tano waliambulia sare na kusepa na pointi tano kwenye msako wa pointi 15 wakiyeyusha pointi 10 mazima.

Miongoni mwa wale waliopata sare dhidi yao ni vigogo Simba ilikuwa Novemba 9, 2022 ubao ulisoma Singinda Big Stars 1-1 Simba, Uwanja wa Liti.

DAKIKA 450 ZA MAUMIVU Ni dakika 450 za maumivu kwao baada ya kuambulia kichapo ndani ya dakika 90. Moja kati ya mchezo ambao walichapwa mabao mengi ilikuwa dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Novemba 17, 2022.

Kigongo kingine ambacho walikutana nacho ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Simba ilikuwa Februari 3, 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 3-1 Singida Big Stars.

Ndani ya dakika 180 ambazo wamecheza Uwanja wa Mkapa na vigogo Simba na Yanga hawajaambulia pointi zaidi ya kutunguliwa mabao 7 huku wao wakifunga mabao mawili.

Hata walipocheza na Azam FC Uwanja wa Azam Complex walipasuka kwa kufungwa bao 1-0 Oktoba 3, 2022.

MABAO 28 Safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 28 kibindoni, mkali wao akiwa ni Bruno raia wa Brazil mwenye mabao tisa pia yupo Meddie Kagere mwenye mabao 7.

Kwenye mabao ya Bruno lipo lile alilomtungua Aishi Manula wa Simba kwa pigo la faulo akiwa nje kidogo ya 18, Uwanja wa Mkapa.

19 Wametunguliwa mabao 19 kwenye mechi 24 ambazo wamecheza wakiwa na wastani wa kutunguliwa bao moja kila baada ya dakika 113 wakiwa uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live