Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio Tanzania tu, Afrika itasimama leo!

Aziz Baleke WA0024 Sio Tanzania tu, Afrika itasimama leo

Sun, 16 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa 11:00 jioni ya leo, sehemu kubwa ya Bara la Afrika itasimama kwa dakika tisini kushuhudia mchezo mkali wa Dabi ya Kariakoo unaotarajiwa kuzikutanisha Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo zinaingia katika mchezo huu zikiwa na kumbukumbu nzuri ya matokeo ya sare ya bao 1-1 mzunguko wa kwanza ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 23, 2022.

Tambo zimekuwa nyingi kwenye vijiwe vya soka mitaani ambapo kila upande umetamba kuibuka na ushindi katika shoo kali inayotarajiwa kushuhudiwa.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema: “Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri, nawajua vizuri wapinzani wetu Yanga, tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa, napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki.”

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, amesema: “Tumejiandaa vizuri na kwa utulivu mkubwa, tunajua kesho (leo) tunakwenda kwenye moja kati ya michezo mikubwa Afrika na siyo kila mara tunacheza mechi inakuwa na mashabiki zaidi ya elfu hamsini, ni lazima tuwatendee haki na tumejiandaa vizuri kwa hilo.

“Kitu kizuri ni kwamba hatuna majeruhi zaidi ya Aboutwalib Mshery ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, wachezaji wengine wote wapo salama.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: