Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sio Luis Miquissone tu... Hata hawa kiboko ya Ahly

Luis Miqusson Pic Data Sio Luis Miquissone tu... Hata hawa kiboko ya Ahly

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author MASHABIKI wa Simba wanatembea vifua mbele kutokana na ushindi ilioupata timu yao dhidi ya Al Ahly jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Huo ulikuwa ushindi wa tatu kwa Simba dhidi ya wababe hao wa soka Afrika, bao pekee lililowazamisha watetezi hao wa michuno hiyo ya Afrika likiwekwa kimiani na Luis Jose Miquissone katika dakika ya 31 ya mechi hiyo ya Kundi A.

Luis alifunga bao hilo lililoipa Simba pointi tatu kwa mguu wa kulia baada ya kuwazidi akili mabeki wa Ahly, lakini limekuwa ni la sita kwa Mafarao dhidi ya timu za Tanzania, kwani kabla ya hapo kuna nyota wengine watano waliowatungua.

Ebu wasome wakali hao waliowahi kuzigusa nyavu za Al Ahly katika mechi mbalimbali za kimataifa, japo timu zao zilienda kutaabika waliporudiana nao kwenye uwanja wao wa nyumbani jijini Cairo, Misri.

MEDDIE KAGERE

Mshambuliaji wa Simba ambaye msimu wa 2018-2019 aliifungia klabu yake bao pekee kwa shuti kali wakati Ahly wakipoteza mchezo wa hatua kama hii walipokutana katika Kundi D na kuipa timu yake ushindi muhimu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz