Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sintofahamu mkataba wa Matampi Coastal

Ley Matampi Pp Sintofahamu mkataba wa Matampi Coastal

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa mye 'clean sheet' nyingi Ligi Kuu Tanzania Bara, Ley Matampi amezua utata juu ya mkataba wake na waajiri wake Coastal Union baada ya pande hizo mbili kutofautiana juu ya urefu wa mkataba huo.

Ipo hivi; Coastal Union, imechimba mkwara kwamba kama kuna klabu inamtaka kipa wao huyo basi waifuate mezani ili wajadiliane kuwauzia kwani Mkongomani huyo bado amebakiza mkataba nao wa mwaka mmoja.

Katibu Mkuu wa Coastal Union Omar Ayoub, ameliambia Mwanaspoti kuwa klabu yao haina shida kwenye kumuuza kipa huyo lakini endapo kuna timu inamtaka mkongwe huyo iwafuate haraka wafanye biashara.

“Ley Matampi ni mchezaji wetu na mkataba wake bado upo, amebakiza mwaka mmoja kama kuna klabu inamtaka basi tunaikaribisha hapa Mkoani Tanga, Barabara ya 11 Ngamiani tutazungumza nao na tukikubaliana tutamuuza, Coastal Union haina shida kabisa kwenye kuuza,” alisema Ayoub.

Wakati Ayoub akiyasema hayo, Matampi ambaye ameongoza kwa kuwa na cleen sheet 15 akimzidi kipa bora wa mara mbili mfululizo Djigui Diarra aliyemaliza na 14, amelithibitishia Mwanaspoti alijiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao umemalizika.

“Hapana,nilisaini mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union sio kweli kwamba nina mkataba zaidi kama kuna timu inanitaka, nikikubaliana nao nitamalizana nao,”alisema Matampi.

“Sijajua kwanini wanasema hivyo lakini tulikubaliana na kusaini mkataba wa mwaka mmoja, huo ndio niliousaini nao.”

Kipa huyo ameiwezesha Coastal Union kumaliza nafasi ya nne msimu huu na kupana nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa, Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika alijiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na waajiri wake FC Lupopo ya Congo.

Chanzo: Mwanaspoti