Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singo''wasilisheni taarifa za wachezajI''

A4cf7405 8be2 4aad B971 5d5613de4d01 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo

Tue, 10 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo amewataka Makocha wanaowaandaa wachezaji kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika michezo ya Kimataifa kuwasilisha taarifa za viwango vyao ili wathibitishwe kuiwakilisha katika michezo hiyo.

Michezo hiyo ni pamoja na ile ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kuanza mwezi Julai 28 hadi Agosti 08, 2022 Burmgham nchini Uingereza na ile ya Dunia kwa mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu mwezi Oktoba, 2022 nchini Uturuki.

Ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei, 2022 wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi pamoja na makocha na mameneja wa timu kilicholenga kupata taarifa za wachezaji sambamba na mambo tofauti ya kufanikisha maandalizi ya timu na wachezaji hao.

"Kuwa na data base za wachezaji ni muhimu ili tuwe na uhakika na matumaini ya uwakilishi wake katika mashindano hayo,"alisisitiza na kuongeza kuwa;

"Tusiikatisha tamaa serikali tujitahidi kushirikiana kwa karibu kukamilisha mambo yetu mapema, lengo letu liwe ni kufanikiwa,"amesema Yusuph Singo.

Kwa upande wao makocha na mameneja wa timu na wachezaji wakiwemo wa mchezo wa Judo, Kuogelea, Ngumi za wazi, wanyanyua vitu vizito vya watu wenye ulemavu na wa mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu wamesema kuwa timu zinaendelea vizuri na mazoezi na changamoto ndogo ndogo zimeendelea kutatuliwa kwa kuwa serikali inatembelea kambi hizo mara kwa mara.

Aidha, timu na wachezaji hao wametakiwa kuendelea na michezo ya majaribio ya kimataifa ili kujiweka vizuri zaidi kabla ya kuelekea katika mashindano hayo ili kuiwakilisha nchi kwa ushindi katika mashindano hayo.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi amewataka viongozi wa vyama hivyo kuwasilisha taarifa muhimu kabla safari ya Burmgham zikiwemo taarifa za chanjo ya Covid

Chanzo: eatv.tv