Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yasajili winga wa Azam

Singida Bs Pic Singida yasajili winga wa Azam

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara litafunguliwa leo Desemba 16, huku kila timu ikipata nafasi ya kuongeza wachezaji wapya kulingana na upungufu wa kikosi chao ili kuimarika kwenye mzunguko wa pili.

Miongoni mwa timu iliyoonyesha nia ya kuboresha kikosi chake ni Singida Big Stars na kuna majina ya mashine mpya nane ambazo zinaweza kutua hapo.

Uongozi wa Singida umeonyesha nia ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao kutokana na upungufu ulioonekana kikosini huku wakitarajiwa kuwamwaga wachezaji tano.

Chanzo cha ndani kutoka Singida kimesema kuwa timu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kumalizana na winga wa zamani wa Azam na Horoya ya Guinea, Enock Atta Agyei ambaye muda wowote atatambulishwa klabuni hapo.

Agyei wakati anacheza kwenye kikosi cha Azam alikuwa miongoni mwa mawinga wasumbufu hadi kusajiliwa na Horoya ambayo msimu huu kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika itacheza michezo miwili dhidi ya Simba.

Katika hatua nyingine uongozi wa Singida inaelezwa upo kwenye hatua za mwisho kumalizana na beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Nickson Kibabage, ambaye tayari ameshaaga kwenye timu hiyo na kueleza anakwenda kuanza maisha mapya kwenye klabu nyingine.

Kibabage licha ya kucheza beki wa kushoto amekuwa akitoa mchango mkubwa kwenye eneo la kushambulia ndio maana hadi mzunguko wa kwanza unamalizika alikuwa ameweka kambani mabao matatu kati ya 21, yaliyofungwa na timu nzima.

Miongoni mwa wachezaji wanaoweza kutolewa kwa mkopo yupo mshambuliaji, Kelvin Sabato anayeweza kwenda kucheza kwenye kikosi cha Polisi Tanzania kilichopo chini ya kocha, Mwinyi Zahera.

Sabato ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara na hadi mzunguko wa kwanza unamalizika alikuwa hajafunga bao lolote.

“Hawa wanaonekana kuwa watasajiliwa lakini Sabato na wengine nafikiri wanne watatolewa aidha kwa mkopo au kuuzwa,” kilisema chanzo.

Chanzo: Mwanaspoti