Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yalazimishwa sare na Ihefu, Kyombo gari limewaka

Singida Vs Ihefu.jpeg Singida yalazimishwa sare na Ihefu, Kyombo gari limewaka

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Singida Big Stars wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.

Mabao yote ya Singida Big Stars yamefungwa na Habib Haji Kyombo dakika ya 31 na 40, wakati ya Ihefu SC yamefungwa na Ismail Mgunda dakika ya 26 na Jaffary Kibaya dakika ya 70.

Kwa matokeo hayo Singida Big Stars inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya tisa, wakati Ihefu SC inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi nane

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: