Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yajibu kupewa jina la Yanga B, Simba B

Onyango Singida FG Singida yajibu kupewa jina la Yanga B, Simba B

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia Klabu ya Singida Fountain Gate kumsajili aliyekuwa beki wa Klabu ya SImba, Joasha Onyango kwa mkopo, Msemaji wa klabu hiyo, @massanzajr amesema;

YANGA B

Tuliposajili wachezaji wengi kutoka Yanga msimu uliopita, ukijumlisha na kupoteza mechi dhidi ya Yanga, tuliitwa Yanga B. Ni maneno ya kukera lakini ndio mashabiki walivyo. Tunavumilia.

SIMBA B

Tunaanza msimu mpya na tayari maneno yameanza kusambaa kwamba Singida ni Simba B. Kisa tu zipo taarifa za chini kwa chini kuwa 'tunapewa' wachezaji na Simba SC.

UKWELI UKOJE?

Ni dhahiri bado watanzania wapo kwenye ulevi wa Simba na Yanga. Sisi kama timu ya kizazi kipya tunaona tunao wajibu wa kubadilisha fikra hizi za kizamani. Ni ngumu lakini tutafanikiwa.

Singida FG tunathubutu kusajili wachezaji bora kutoka vilabu vyote ndani na nje ya nchi kulingana na mahitaji yetu. Timu yetu ni chotara. Tutasajili bila kujali wanazi wa soka watasemaje, malengo yetu kwanza.

Tumedhamiria kuleta ushindani ligi kuu na hata kimataifa. Ni dhamira inayopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ya soka. Ushabiki wa kizamani hauna nafasi tena. Tutazame picha kubwa.

Maendeleo hayana chama!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live