Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yaikalia kooni Azam FC

Singida Hj Singida yaikalia kooni Azam FC

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Singida Big Stars imetamba imejiimarisha tayari kusaka matokeo mazuri kwa lengo la kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kwa sasa Singida Big Stars ipo katika nafasi ya tatu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ihefu ikiwa imepishana pointi moja na Azam FC yenye alama 43.

Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Massanza, alisema wamefurahishwa kuona wameishusha Azam FC na sasa wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanabakia katika nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu.

Massanza alisema anafahamu ushindani uliopo katika mechi za ligi, lakini wachezaji wao wameahidi kujituma katika kila mechi watakayocheza.

"Tumefanikiwa kupata alama moja baada ya sare na Ihefu imetusaidia kuvuka daraja na kupanda nafasi ya tatu, kazi nzuri hii ni kutokana na matokeo mazuri na pointi moja tuliyoipata ingetusaidia kufika nafasi ya tatu na kuishusha Azam. Tunaendelea kupambana kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote zilizobakia ili kumaliza ligi katika nafasi ya tatu ya msimamo, timu ina ari kubwa katika michezo iliyobakia.

"Tumerejea nyumbani kutoka Mbeya tumewapa mapumziko wachezaji kwa ajili ya kukaa sawa, ukiangalia mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar upo mbali (Februari 27, mwaka huu), hivyo tumeona tuwape mapumziko mafupi hadi Ijumaa, tutaanza maandalizi kuelekea mchezo huo Jumamosi (kesho)," alisema Massanza.

Wakati huo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kalimangonga Ongala, amesema mechi mbili za kirafiki walizocheza zimempa mwanga na kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa heshima.

Kalimangonga alisema wanatarajia kupata matokeo chanya kuanzia mechi ijayo dhidi ya Simba na nyingine zilizobakia katika ligi hiyo ya juu nchini.

Azam FC itakuwa na Simba katika mchezo wa raundi ya 24 ya Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Februari 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live