Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yaigomea Simba kwa Miquissone na Phiri

Miquissone Phiriii Singida yaigomea Simba kwa Miquissone na Phiri

Tue, 16 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Singida Fountain Gate imeitupilia mbali ofa ya Simba kuwapa winga Luis Miquissone na Mosses Phiri ili wamnase kiungo Marouf Tchakei.

Simba ilikuwa tayari kuwatoa mastaa wake hao wawili kwa Singida FG ikionyesha kuhitaji sana saini ya kiungo huyo raia wa Togo anayejua kuchezesha timu na hata kufunga.

Simba imekubaliana kila kitu na Tchakei kupitia meneja wake lakini mkataba wa kiungo huyo na Singida FG ndio umekuwa kikwazo.

Singida FG Imewaambia Simba haijafika kwenye kina cha pesa inachotaka na wala haiwahitaji Phiri na Miquissone.

Ndani ya hilo Phiri mwenyewe amewasisitizia Simba kuwa hataki kutoka kwa mkopo na kama hawamtaki njia rahisi ni kusitisha mkataba huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live