Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida waitembezea kichapo Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri

IMG 7648.jpeg Singida waitembezea kichapo Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Ijumaa Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na kiungo Morice Chukwu dakika ya na saba na beki Augustino Samson aliyejifunga dakika ya 13, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na Paul Peter Dalila ya 64.

Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate wanafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya tano, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 15 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: