Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida waitembeza kichapo Mashujaa Kigoma

Singida Big Stars Kigoma.jpeg Singida waitembeza kichapo Mashujaa Kigoma

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara novemba 6 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na Gardiel Michael dakika ya 18, Marouf Tchakei dakika ya 44 na Habib Kyombo dakika ya 64, wakati bao pekee la Mashujaa FC limefungwa na Adam Adam dakika ya 85.

Kwa ushindi huo Singida Big Stars inafikisha pointi 12 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya saba, wakati Mashujaa FC wanabaki na pointi zao nane za mechi nane nafasi ya 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live