Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida waichimbia Shimo Polisi Tz Uwanja wa Liti

D096D92F 2598 4383 AEDF 7824B790D3C9.jpeg Singida waichimbia Shimo Polisi Tz Uwanja wa Liti

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.

Mabao ya Singida Big Stars leo yamefungwa na mabeki Pascal Wawa dakika ya 13, Nickson Kibabage dakika ya 57 na mshambuliaji Amissi Tambwe dakika ya 90.

Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 26, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikiizidi pointi nne Azam FC ambayo usiku wa leo inacheza na Mtibwa Sugar.

Hali inazidi kuwa mbaya kwa Polisi baada ya kichapo cha leo, kwani inaendelea kushika mkia ikibaki na pointi 19 za mechi 26 sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live