Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida waichapa Coastal Union Uwanja wa Liti

IMG 7715.jpeg Singida waichapa Coastal Union Uwanja wa Liti

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Singida Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Unión katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa LITI mjini Singida.

Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 30 na beki Mkongo Felly Mulumba aliyejifunga dakika ya 52, wakati bao pekee la Coastal Unión limefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid dakika ya 72.

Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nne, wakati Coastal Unión inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: