Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida waanza na moto Kombe la Shirikisho Afrika

IMG 5412.jpeg Wachezaji wa Singida FG wakishangilia mabao yao mchezo dhidi ya JKU

Sat, 19 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Singida Fountain Gate ‘Big Stars’ imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusogea mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKU ya Zanzibar jana Agosti 18 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na viungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya nne na 39 yote kwa penalti, Mnigeria Maurice Chukwu dakika ya 44 na Duke Abuya dakika ya 47, wakati la JKU limefungwa na Saleh Abdullah kwa penalti pia dakika ya 63.

Timu hizo zitarudiana Agosti 27 hapo hapo Azam Complex na mshindi wa jumla atamenyana na Future ya Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live