Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida vs Simba: Mashabiki wakosa pa kukaa Liti

Liti Pic Singida vs Simba

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda mchache kabla ya kuanza mchezo wa Ligi Kuu kati ya Singida Big Stars na Simba Sc katika uwanja wa Liti mashabiki wamekosa sehemu ya kukaa kutokana na uwanja kujaa.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na timu hizo kushinda michezo yao ya mwisho.

Kutokana na VIP na mzunguko kujaa mashabiki hao wamekaa nyuma ya magoli wakiwa hawajui waende wapi.

Baadhi wameonekana wakiwa na miamvuli huku wakilalamika kulipia tiketi na kukosa sehemu za kukaa.

Juma Misung'aa alisema waliopo nje ya uwanja ni wengi kuliko walioko ndani lakini wanashangaa wahusika kuendelea kukata tiketi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live