Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida kuliamsha Mapinduzi Cup 2024

Singida Big Stars Kigoma.jpeg Kikosi cha Singida Big Stars

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Singida Fountain Gate iliyohamishia kwa muda maskani jijini Arusha kwa mechi za nyumbani kutokana na Uwanja wa Liti, mkoani Singida kufungiwa, imethibitisha itashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 inayofanyika visiwani Zanzibar.

Msimu uliopita wa michuano hiyo, Singida ilicheza fainali dhidi ya Mlandege iliyobeba ubingwa kwa ushindi wa mabao 2-1 na mapema leo mchana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Massanza amethibitisha juu ya ushiriki wao kwa msimu mpya baada ya kupata mualiko rasmi.

"Tumepokea mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) na tayari tumeingiza kwenye ratiba zetu kumbukeni, tulimaliza nafasi ya pili ya msimu uliopita, hivyo wakaona ni busara kutualika, nasi tumeupokea mwaliko huo," amesema Massanza.

Kuhusu mechi za nyumbani baada ya Uwanja wa Liti kufungiwa, Massanza amesema zote zitachezwa Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu, jijini Arusha zikiwamo mechi za Ligi Kuu dhidi ya KMC na ule wa Kombe la Shirikisho (ASFC) ikipangwa kupigwa Desemba 15 dhidi ya Arusha City,

"Kikubwa tulikuwa tunaangalia maeneo ya jirani ambayo Wanasingida, wanaweza kufika na baada ya machaguo yote hatimaye tukaupata Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu, Arusha,” amesema Massanza aliyefafanua mara baada ya mechi hizo, timu ndipo itasafiri kwenda Zanzibar.

Chanzo: Mwanaspoti