Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Utd yaanika jeshi lake jipya TPL

69538 Singida+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MABOSI wapya wa Singida United wametangaza kikosi chao kipya kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ambacho kwa asilimia kubwa kimeonekana ni kikosi cha kujilisha zaidi.

Singida imetaja kikosi cha nyota 30 huku kati ya hao kumi ni walinzi na walinda milango watatu, viungo nane wakati washambuliaji wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji tisa.

Kwa mujibu wa kikosi hicho inaonyesha benchi la ufundi lililo chini ya Kocha Fred Felix Minziro limedhamiria kujilinda zaidi akizungumza na Mwanaspoti, Kocha huyo alisema usajili wao umezingatia mahitaji.

"Hakuna timu ambayo haisajili safu ya ulinzi kusajili nyota wengi katika eneo hilo haina maana kwamba wachezaji waliosajiliwa katika safu ya ushambuliaji watakuwa hawana majukumu," alisema Minziro na kuongeza;

"Kikubwa ninachoweza kukwambia tukutane msimu ujao usajili huo uliouona ndio utakaotoa majibu ni kwanini na wao wamesajili idadi hiyo na kuongeza kuwa maandalizi kuelekea msimu huo mpya yanaenda vizuri na wanajiandaa ili kushindana."

Katika msimu uliopita ukiwa wa pili kwao, Singida United ilimaliza katika nafasi ya 13 ikikusanya pointi 46 kutokana na mechi 38, lakini ikiwa ni baada ya kupigana kuepuka kushuka daraja.

Chanzo: mwananchi.co.tz