Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Utd bado mambo magumu

90898 Singida+pic Singida Utd bado mambo magumu

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

MABAO mawili yaliyowekwa kimiani na Sadalla Lipangile wa KMC yalizidi kuiweka pabaya Singida United katika Ligi Kuu Bara.

KMC ilipasha ushindi huo kwenye mfululizo wa Ligi Kuu mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini hapa ambao Singida wanautumia kama wa nyumbani baada ya Namfua (sasa Liti) kufungiwa na TFF.

Kipindi hicho kimeifanya Singida kuzidi kujikita mkiani ikiwa na alama zao saba tu katika mechi 15, lakini KMC wakiongeza alama tatu zinazowafanya wafikishe pointi 13, japo haijawasaidia kuondoka nafasi ya 17 waliyokuwepo baada ya mechi za Jumamosi.

Katika mchezo huo wa raundi ya 15, Singida iliyo chini ya Kocha Ramadhan Nswanzurimo iolionekana haijapata dawa ya kujikwamua mkiani kwani, licha ya kufanya mashambulizi mengi, lakini ilishindwa kukwamisha mipira nyavuni.

Washindi KMC ambao huo ni ushindi wao wa kwanza tangu NOvemba 4 mwaka jana walipoifunga Biashara United na kucheza mechi zaidi ya sita bila kuonja ushindi.

Lipangile alifunga mabao yake katika dakika ya 12 na 78 na kuwanyamazisha wenyeji wao, Singida United ambao kama hatajikwamua huenda wakarudi Ligi Daraja la Kwanza.

Ligi hiyo itaendelea tena Jumatano kwa michezo kadhaa, huku vigogo Simba na Yanga waliotoshana nguvu jana katika derby, watakuwa wakikinukisha kwenye Kombe la Mapinduzi inayoanza kesho visiwani Zanzibar.

Chanzo: mwananchi.co.tz