Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida United yaomba huruma ya wananchi

Singida+pic Singida United yaomba huruma ya wananchi

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertUONGOZI wa Singida United umewataka watu wote wa mkoa huo  kuiunga mkono timu yao ili iweze kufanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na kurejea Ligi Kuu kwa kishindo msimu wa 2021/2022.

Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrhman Sima  amesema kitu kikubwa kilichoiangusha timu hiyo kwenye ligi ni kukosa sapoti kutoka kwa wakazi wa mkoa huo na timu kuachwa kwa baadhi ya watu pekee.

Amesema hivi sasa wanatakiwa kutafuta wadhamini ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye FDL na kurejea ligi kuu.

"Hivi sasa tunatakiwa kukaa na kuona wapi tulikosea lakini kubwa ni kutafuta wadhamini kwani mpira ni pesa na ukikosa pesa mambo hayawezi kwenda kwani kuendesha timu ni gharama kubwa.

"Tunatakiwa kuwa na umoja kwa wanasingida wote tusipofanya hivyo timu inaweza kushuka mpaka ngazi ya Wilaya hivyo lazima watu waamke na kuipenda na kuisapoti timu yao.

"Ukiangalia jambo lililoigharimu timu hii kwenye ligi msimu uliomalizika ni kukosa sapoti ya wadau wa soka na wananchi kwa ujumla kwani wengi walikuwa wakizishangilia timu kubwa tu Simba, Yanga na Azam lakini walisahau  kuwa uwepo wa Singida United unawanufaisha wananchi wengi wa mkoa huu kibisahara kwani timu hizo zikija, hoteli, usafiri na hata biashara nyingine watu wanavuna pesa", amesema Sima.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz