Kikosi cha Singida Fountain Gate FC tayari kipo nchini Misri kucheza dhidi ya Future FC mchezo wa marudiano kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF
Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate FC Masanza amekiri kuwa bado timu haina Kocha Mkuu lakini amesema hilo si tatizo kwa sababu wana benchi la ufundi lenye makocha na wataalam wa kutosha.
"Timu imesafiri ikiwa na jumla ya wachezaji 23 pamoja na benchi la ufundi na baadhi ya viongozi (Rais, Makamu wa Rais, Mtendaji Mkuu n.k)."
"Tunalo benchi la ufundi ambalo limesheheni makocha wa kutosha pamoja na wataalam wengine wenye uzoefu."
"Suala la Kocha wetu linafahamika bado halijakaa vizuri lakini hiyo haituzuii sisi kufanya vizuri, hata kama Imamu hayupo ibada lazima ziendelee."
"Benchi la ufundi linaendelea na kazi yake ya kuiandaa timu ambayo ilianzia nyumbani Tanzania."
Mechi kati ya Future FC dhidi ya Singida Fountain Gate FC inatarajiwa kuchezwa Oktoba 1, 2023 huku Singida Fountain Gate FC ikiwa na faida ya ushindi wa goli 1-0 ilioupata kwenye mchezo wa kwanza nyumbani [Azam Complex, Chamazi].