Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Fountain Gate yamtambulisha Kasano

Kasano Singida Singida Fountain Gate yamtambulisha Kasano

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Meneja wa Bodi ya Ligi Kuu, Jonathan Kasano ametambulishwa rasmi katika klabu ya Singida Fountain Gate akiwa kama Ofisa mkuu wa oparesheni zote za timu hiyo.

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Olebile Sikwane amesema wamemuongeza Kasano kwa sababu ana uzoefu mkubwa katika soka la nchini na hata kimataifa.

“Ana uzoefu wa nje ya nchi na hapa ndani kwani ameshafanya kazi TFF na Bodi ya Ligi hivyo atatusaidia,” amesema Sikwane.

Sikwane ameongeza akisema; “Kasano amefanya kazi kwenye Ligi hivyo na jinsi ambavyo ratiba imebana tunaamini kabisa atatusaidia,”

Upande wa Kasano amesema hana maneno mengi badala yake ni utaendaji na tayari ameshaanza kazi yake.

Kasano amesema wana mechi ya CAF na kama mtendaji wamekamilisha kwa hatua kubwa mahitaji yote yanayohitajika kwenye mchezo.

“Viongozi wa CAF wameshaingia, wageni wetu kutoka Zanzibar wameshaingia pia na usiku leo waamuzi watafika;

“Mechi za CAF zinahitaji maandalizi makubwa na kwa kiwango kikubwa tumekamilisha kwenye upande wa maandalizi,”

Kasano ameutumikia mpira wa nchini kwa miaka sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: