Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG yashikilia kibarua cha Kaze

Cedrick Kazeeee Kocha Mkuu wa Namungo, Cedrick Kaze

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Namungo, Cedric Kaze baada ya kuiongoza timu yake kwa mechi tano akikusanya pointi tatu na kupoteza kumi amesema mchezo dhidi ya Singida Big Stars umeshikilia hatma yake, hivyo anahitaji pointi tatu.

Namungo kwenye mechi tano ilizocheza imepoteza mbili na kutoka sare tatu ikianza na Kagera Sugar (1-1), Mashujaa (0-0), Yanga (1-0), KMC (1-1) na walikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Akizungumza Kaze ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga alisema anaingia kwenye mchezo dhidi ya SBS akiwa na uhitaji wa pointi tatu muhimu kwa lengo la kujihakikishia kibarua chake ndani ya timu hiyo.

Kaze alisema anatambua umuhimu wa pointi hizo, mbali na kibarua chake kuwa rehani anatakiwa kujitengenezea CV nzuri ambayo itambeba katika majukumu yake nje ya Namungo ambayo pia amekiri kuipambania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: