Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG yaiwahi Yanga mapema Dar

Singida FG Dar Es Salaam Msafara wa Kikosi cha Singida FG

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikiwa na kibarua kesho cha kupambana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, wap-inzani wao wengine Singida Big Stars watakaokutana nao Ijumaa hii tayari wamewasili salama jijini Dar es Salaam wakitokea mjini Lindi kwa ajili ya maandalizi.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Singida katika mchezo mkali kutokana na ubora wa timu zote mbili huku mabingwa hao watetezi wakiwa na rekodi ya ushindi wa mabao 4-1, mara ya mwisho walipokutana Novemba 17, mwaka jana, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha msaidizi wa timu hiyo, Thabo Senong amesema licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo ila kitendo cha kupata matokeo chanya kutoka kwa Namungo kimewaongezea morali wachezaji cha kuendelea kupambana zaidi.

“Kila mchezo ni mgumu lakini maandalizi bora siku zote ndiyo yanayoamua, kwetu ni changamoto nyingine iliyopo mbele yetu ambayo tunakabiliana nayo, tunaiheshimu Yanga ila hatutakuja kinyonge kwani tunahitaji kupata pointi tatu pia,” amesema.

Kwa upande wa beki wa timu hiyo, Carno Biemes alisema ushindani umekuwa ni mkali katika kila mchezo wa Ligi Kuu, hivyo wachezaji wanatambua mashabiki zao wanahitaji nini na jukumu wanalo-paswa kulifanya kwa ubora kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

Huu utakuwa ni mchezo wa tatu kwa Singida kukutana na Yanga katika Ligi Kuu Bara na haijawahi kushinda kwani licha tu ya kupoteza kwa mabao 4-1 Novemba 17, mwaka jana ila mchezo wa mwisho uliopigwa Uwanja wa Liti Mei 4, mwaka huu timu hiyo ilichapwa 2-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: