Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG wawawinda JKU Kimataifa

Afisa Habari Wa Singida Singida FG wawawinda JKU Kimataifa

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida FG wameweka kambi yao jijini Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa Kimataifa dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Akizungumzia maandalizi yao, Afisa Habari wa Singida FG, Hussein Msanza, amesema anawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwashangilia ili waweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Agosti 18, 2023.

"Msimu huu tuna majukumu makubwa sana, kabla ya Ligi Kuu tunaanza na michuano ya Kimataifa Kombe la Shirikisho, tunaanza na JKU mchezo tutakaocheza hapahapa Dar na kisha tukifanikiwa kuvuka kuhunzi hicho tutacheza na The Future ya Misri,” alisema Masanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live