Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG wanarejea kujipanga upya

Singida Res.jpeg Singida FG wanarejea kujipanga upya

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Future FC ya Misri imewafungashia virago Singida Fountain Gate ya Tanzania katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Oktoba Mosi, 2023 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Al Salaam, ulisoma Future 4-1 Singida Fountain Gate.

Bao pekee la Singida Fountain Gate lilipachikwa na nyota Marouf Tchakei kwenye mchezo huo ambao Singida Fountain Gate walikuwa na faida ya bao moja waliloshinda Uwanja wa Azam Complex.

Licha ya wachezaji wa Future kuwa pungufu kwa kuwa mmoja alionyeshwa kadi nyekundu bado mbinu zao zilikuwa ngumu kuvunjika mbele ya Singida Fountain Gate waliokuwa wakipambana kuandika rekodi mpya kutinga hatua ya makundi.

Mwendo umegota mwisho wanarejea nyumbani kujipanga kwa mechi zijazo za ligi na mashindano mengine.

Ni Beno Kakolanya kipa namba moja wa Singida Fountain Gate alikuwa langoni kwenye mechi zote mbili ile ya Dar na iliyochezwa ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live