Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG wanaporomoka kama utani

Makocha Singida Singida FG wanaporomoka kama utani

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maisha yameenda kasi sana kwa Singida Fountain Gate na hili linapaswa kuwa fundisho tosha katika soka letu katika namna ya kuendesha timu zetu.

Ilipata nafasi kwa kununua nafasi ya timu iliyokuwa inaitwa DTB wakati huo ilikuwa katika Ligi Daraja la Kwanza ambayo hivi sasa inafahamika kama Ligi ya Championship.

Kigogo aliyekuwa anaimiliki nasikia ni mzito sana na ana wadhifa mkubwa serikalini hivyo akasajili wachezaji mastaa wa ndani na wa kigeni wakaenda kuichezea pasipo kujali kama ipo Ligi Daraja la Kwanza, muhimu ni fedha tu.

Ikafanikiwa kupanda na ilipoingia Ligi Kuu ikabadilisha jina na kuanza kuitwa Singida Big Stars huku ikizidi kukusanya wachezaji mastaa tena ikipora wengine ambao walikuwa wanawaniwa na watani wa Kariakoo.

Unaposajili wachezaji wenye majina na gharama kubwa maana yake unatengeneza mazingira ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kulipa mishahara na stahiki nyingine za wachezaji na pia kulipa gharama kubwa za fedha kuvunja mikataba yao.

Kwa bahati mbaya kuna wachezaji hasa wa kigeni wakawa wanaachwa huku wakiwa wanaidai klabu na hivyo wakashawishika kwenda kushtaki katika vyombo vya kimataifa vya soka ambavyo viliona wana haki na kuilazimisha klabu kulipa hizo stahiki jambo lililoiacha katika madeni makubwa.

Sasa inasemekana yule kigogo akaamua kuiacha na kununua timu nyingine huku akihamisha wachezaji tegemeo jambo ambalo limeanza kuiathiri timu.

Tangu mabadiliko hayo yalipoanza kutokea, Singida imekuwa ikipitia kipindi kigumu na haijaweza kushinda mechi hata moja ya Ligi Kuu hadi sasa.

Na ndio maana imekuwa sio ajabu kuona ikitoka nafasi za juu na sasa inakaribia kuingia katika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa ligi.A

Chanzo: www.tanzaniaweb.live