Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG wamlilia Kibabage

Kibabage Vs Medeama.jpeg Singida FG wamlilia Kibabage

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa @singidafountaingate, Hussein Massanza @massanzajr ameonesha kujutia mauzo ya beki wa pembeni Nickson @kibabage__no3 kwenda Yanga katika dirisha la usajili la mwezi Julai, 2023.

@massanzajr ameshindwa kujizuia hisia zake baada ya ukurasa wa Meneja Habari na Mawasiliano wa @yangasc, Ally Kamwe @alikamwe kuchapisha taarifa za kukoshwa na kiwango cha kinda wao @kibabage__03

"Wakati timu nyingine mabeki wao ni 'kauka nikuvae'. Wananchi ndio kwanza tunamfaidi @kibabage__03 ," imeeleza taarifa hiyo.

@kibabage__03 mwenye mkataba wa miaka miwili na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara amekuwa katika kiwango bora, licha ya ushindani wa namba kati yake na mkongwe Joyce Lomalisa kutoka DRC.

Ubora wa kinda huyo umemshawishi Kocha wa @taifastars, Adel Amrouche kumjumuisha katika kikosi cha wachezaji 53 wa awali Stars kwaajili ya maandalizi kuelekea Fainali za Mataifa Afrika zinazotarajiwa kuanza Januari 13, 2024 nchini Ivory Coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live