Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG matumaini kibao kwa kocha Middendorp

Image 86.png Matumaini kibao kwa kocha Middendorp

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa mchezo wa kwanza kwa kocha wao mpya, Ernst Middendorp utakuwa ni wa kimataifa na wana matumaini watapata ushindi.

Kocha Mkuu Middendorp amechukua mikoba ya Hans van Pluijm ambaye hatakuwa na timu hiyo kwa msimu wa 2023/24 baada ya kupewa kwaheri.

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza amezungumza jijini Dar es salaam na kusema kuwa maandalizi ya kikosi chao yanaendelea vizuri na wana matarajio makubwa na kocha huyo kutoka nchini Ujerumani.

Mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Future utakuwa ni wa kwanza kwa kocha wetu mpya na tunaamini atafanya vizuri na tutapata matokeo.

Kikubwani mashabiki kuwa pamoja nasi kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu na utakuwa ni wa kwanza kwa kocha wetu mpya ambaye ameanza kuwapa mbinu wachezaji.

Chanzo: Dar24