Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG kufunga mahesabu na JKU leo

Singida Fountain Gate Tizi Singida FG kufunga mahesabu na JKU leo

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 katika mchezo wa mwanzo dhidi ya JKU, Singida Big Stars leo itakuwa na kibarua rahisi cha kusaka tiketi ya kutinga raundi ya kwanza wakati itakaporudiana na wawakilishi hao wa Zanzibar katika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:30 usiku.

Singida Big Stars wanahitaji ushindi, sare au kutopoteza kwa tofauti ya zaidi ya mabao mawili ili itinge katika hatua inayofuata ambayo itakabiliana na Future ya Misri, kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumzia mchezo huo, kocha mkuu wa JKU, Salum Ally Haji alisema wapo kwenye wakati mgumu kwa sababu ya matokeo mabaya waliyopata katika mechi ya kwanza na wanategemea miujiza tu leo.

"Sisemi tunaenda kufuzu ila tunaamini tunaenda kushinda mchezo huu, mabao manne ni mengi sana kwenye mpira lakini nimekiandaa kikosi changu kupata matokeo," alisema Haji.

Kocha wa Singda BS, Hans Pluijm alisema licha ya ushindi mnono walioupata katika mechi ya kwanza,amewatengeneza kisaikolojia wachezaji wake ili wasibweteke leo.

"Tunatakiwa tusiamini kwamba tumeshafika sehemu ambayo tunaitaka. Yale matokeo ya kwanza tumeshasahau na sasa tunataka ushindi kwenye mchezo huu,"alisema Pluijm.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live