Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG: Tumeuza wachezaji ili tulipe madeni

Tchakeiii Qwd Singida FG: Tumeuza wachezaji ili tulipe madeni

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate, Japhet Makau amesema kuwa Klabu hiyo imeamua kuuza baadhi ya wachezaji wake ili kupata fedha za kulipa madeni waliyokuwa wakidaiwa.

Singida FG ni klabu ambayo ilinunuliwa kutoka Singida Big Stars kabla ywa msimu huu kuanza na imekuwa ikifanya vizuri na kutoa ushindani mkubwa kwa vilabu kongwe hapa nchini katika Ligi Kuu na michuano mingine ambayo imekuwa ikishiriki.

Akizungumza na wanahabari jana, Makau amesema; "Ni kweli tumeuza baadhi ya wachezaji wetu ili kupata fedha za kulipa madeni ya klabu.

"Wenzetu kutoka klabu kubwa ndani na nje ya nchi walileta ofa zao na tukakaa nao mezani. Wapo waliofikia kiasi tulichotaka ndio hao tumefanya nao biashara. Wengine ofa zao hazikutosha.

"Tulikuwa na wachezaji wazuri wenye ubora wa hali ya juu takribani 40. Hivyo hakuna athari yoyote tutakayoipata kwa kuuza wachezaji wachache. Bahati nzuri tulisajili wachezaji ambao ubora wao haupishani kwenye nafasi wanazocheza," amesema Makau

Wachezaji ambao mpaka sasa wameachwa na Singida FG baada ya dirisha dogo ni Gadiel Michael (ambaye ametimkia Afrika Ksuini), Meddie Kagere (amekwenda Namungo), Marouf Tchakei (28) raia wa Togo, Duke Abuya (29) raia wa Kenya na golikipa Khomeiny Khomeiny.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live