Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG: Tumerejea na nguvu mpya

Namgungo Vs Singida Singida FG: Tumerejea na nguvu mpya

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Singida Fountain Gate kimeendelea na mazoezi ya kujiwinda na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC, huku uongozi wa timu hiyo ukisema wamerejea na nguvu mpya.

Mchezo ujao, Singida itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi kucheza dhidi ya Namungo FC, keshokutwa Jumamosi (Oktoba 21).

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hassan Masanza, alisema: “Tumerejea na nguvu mpya ya kuwawinda Namungo FC, maandalizi yanaendelea vizuri kabisa, kikubwa tumepata Kocha Mkuu mpya Ricardo Ferreira, tuna imani ana uwezo wa kushindana kwenye levo moja na timu zinazoshikilia nafasi ya kwanza na ya pili Tanzania.”

Singida Fountain Gate mpaka sasa wameshacheza mechi tano kwenye Ligi Kuu Bara, wapo nafasi ya 9 na pointi 5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live